Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Chasherehekea Miaka 20 Tangu Kuanzishwa Kwake

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimeadhimisha miaka ishirini (20) tangu kilipoanzishwa rasmi mwaka 1992. Kilele cha maadhimisho hayo kilifanyika tarehe 28/10/ 2012 katika mahafali yaliyofanyika katika makao makuu ya kudumu yalioyopo Bungo, Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Mkuu wa Chuo Dk. Samwel Malecela amesema kwamba, lengo la OUT ni kuona kuwa kila mwananchi anapata elimu ya juu bora zaidi na kwa gharama nafuu popote pale alipo na itakayomfaa kwa mazingira yake ya maisha, ajira au kujiajiri mwenyewe na wenzake.

Amesema, nia ya dhati ya serikali ni kuwapatia watanzania masikini, akina mama wenye mapungufu mbalimbali ya kuzaliwa nayo au hata ya kutokea ukubwani.

Katika miaka 20 iliyopita, chuo chetu, chuo chetu kimewafikia kutoka vituo vichache wakati kilipoanzishwa mwaka 1992 na kuanza udahili mwaka 1994 ambapo anasema chuo kina vituo vya mikoa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kasoro mkoa mmoja mpya, anasema Dk. Malecela na kuongeza kuwa sasa OUT ina vituo vya uratibu katika nchi za Kenya, Rwanda na Namibia.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Tolly Mbwette alisema wao kama jumuia ya Chuo hicho, wanaona uzinduzi wa maadhimisho hayo ni tendo kubwa sana ambalo linafanya ile ndoto ya muasisi wa taifa letu Mwl. Julius K. Nyerere ambaye pia ni muasisi wa wazo la kuanzishwa chuo hicho iwe kweli.

Alisema, ndoto hiyo ya Mwalimu iko katika maneno aliyosema, namnukuu ” sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike mpaka nje ya mipaka yetu, ulete tumanini” mwisho wa kumnukuu. Profesa Tolly Mbwette anasema wana imani kubwa kuwa OUT kimetekeleka kwa mafanikio makubwa ndoto hii ya  Mwalimu Nyerere ambapo sasa hivi chuo kina vituo nchi nzima na pia kina ofisi za uratibu katika nchi kadhaa kama vile Kenya, Rwanda na Namibia.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Tanzania Profesa Samwel Wangwe amesema katika kipindi chote cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa  Chuo Kikuu cha Tanzania, baraza la chuo ndio chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwenye muundo wa utawala wa chuo, limesimamia mageuzi na maendeleo mengi yaliyofikiwa na chuo hicho hatua kwa hatua

Anasema, baraza la chuo limejitahidi, kuendesha chuo kwa mafanikio makubwa ikiwemo kusimamia kwa kina utekelezaji wa sheria namba 17 ya mwaka 1992 iliyoanzisha chuo hicho miaka 20 iliyopita.

Profesa Wangwe anafafanua kuwa hata hivyo, kutokana na kukua na kuongezeka kwa mahitaji ya jamii yetu ya kitanzania na pia kuongezeka kwa changamoto, chuo kilibadili sura yake na hasa baada ya kupitishwa kwa sheria ya Vyuo vikuu namba 7 ya mwaka 2005 ambapo ilibidi kuanzia tarehe 1, January, 2007 chuo kiendeshwe kufuatia hati idhini ya chuo ya mwaka 2007.

Sheria hiyo ndiyo iliyoleta mageuzi makubwa ya elimu hapa nchini. Alisema, Baraza lilisimamia mchakato wa kutengeneza hati indini ya chuo ambayo ndiyo sheria inayokiendesha chuo hadi sasa ambapo chini ya hati idhini, baraza limeshuhudia mabadiliko makubwa kabisa ya kiutendaji yakitokea chuoni hapo, mifumo ya utoaji huduma ikiimarishwa na sera miongozo mbalimbali ya kusimamia uendeshaji wa chuo ikitengenezwa.

Ameongeza kuwa matokeo yake chuo kimeongeza udahili na kuwa chuo chenye kudahili wanafunzi wengi hapa nchini katika masomo ya shahada za kwanza, uzamili na uzamivu. Mwenyekiti huyo wa baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, anasema pamoja na hayo, baraza lilipitisha Mpango Mkakati wa 2010/2011- 2014/2015 ambao hutoa dira ya dhima ya chuo.

Amesema kupitia mkakati huo, chuo kimeweza kujipangia malengo na kusimamia utekelezaji ambao umetokana na mafanikio yaliyopo katika kuadhimisha miaka 20 tangu chuo hicho kianzishwe.

 Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Samwel malecela, akitoa hotuba katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Chuo.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Tolly Mbwette, akitoa hotuba katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Chuo.

Kutoka Kushoto, Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Samwel Wangwe, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dk. Samwel Malecela na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Tolly Mbwette wakiteta jambo katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 tangu Chuo Kuanzishwa.

Raisi wa awamu ya pili, Dk. Ally Hassan Mwinyi, akizindua kitabu cha historia ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa chuo.

 

Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Samwel Wangwe, akitoa hotuba katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 na mahafali ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika katika viwanja vya Bungo, kibaha, Pwani.

Waziri katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, ndugu Shamhuna, akitukiwa shahada na mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzaia, Dk. Samwel Malecela

 

Mkuu wa idara ya maktaba, Dk. Athumani Samzugi, mara baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari wa Falsafa (Doctor of Philisophy) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Wahitimu wa shahada ya udaktari (PhD). Kulia ni Dk. Athumani Samzugi wa idara ya Maktaba, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Dr. Jerome Chilumba

Baadhi ya wahitimu wa kwanza wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Kutoka kulia ni ndugu Gasper Munisi

Baadhi ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Kutoka Kulia ni Dk. Pius Ng’wandu na Ndugu William Lukuvi

Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Mmoja wa wafanyakazi waanzilishi wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania, akipewa zawadi na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda

Baadhi ya wageni waalikwa katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s